Monday, November 30, 2015

Bomoabomoa yaendelea Dar, unawezaje kukwepa nyumba yako isibomolewe? majibu yako hapa.


Zoezi la kubomoa nyumba na majengo yaliyoingia ndani ya hifadhi ya miundombinu ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini, limeendelea mwishoni mwa wiki ambapo baaadhi ya nyumba zilizokuwa zimejengwa ndani ya maeneo hayo ya Salasala zimevunjwa.
01 copy
Katapila likiwa ndani ya gari tayari kwa kazi ya bomobomoa eneo la Salasala ,Dar es salaam 
Watu wengi wamekuwa hawaelewi vigezo vinavyozingatiwa hususani umbali sahihi wa mtu kujenga nyumba yake, hapa Mkurugenzi wa usimamizi na ufundi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang’ingo  anaeleza>>
Umbali sahihi unaopaswa wakazi hao kujenga makazi yao kutoka lilipo bomba la maji ni mita 15 kila upande ambapo hatua hiyo inapelekea kuwa jumla ya mita 30 ya umbali unaotakiwa
ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama na kuruhusu matengenezo mengine tofauti na hali ya awali ambayo huwezi hata kufanya kazi maana bomba limepita ndani ya uzio na makazi ya watu ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha yao na mali zao”;-Romanus Mwang’ingo
Maeneo yaliyohusishwa na ubomoaji huo ni pamoja na Bunju, Bondeni, Boko, Tegeta, Mbezi Intacheki, na Mbezi Tangibovu ili kuruhusu kukamilisha ujenzi wa bomba hilo la maji kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam.
02 copy
09 copy
Baadhi ya wakazi wa eneo la Salasala, Dar es salaam wakishuhudia zoezi la bomoabomoa
10 copy

No comments:

Post a Comment