ICC yapunguza kifungo cha Katanga
Majaji wa rufaa
katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC wamepunguza hukumu
aliyopewa kiongozi wa zamani wa waasi nchini Congo Germain Katanga.
ICC imesema kifungo cha Katanga kilichokuwa miaka 12 kitapunguzwa kwa miaka mitatu na miezi minane.Majaji wamefanya uamuzi huo kwa kuwa alisema anajutia matendo aliyoyatenda, anajitenga na uhalifu uliofanywa na wanaona kwamba anaweza akatafutiwa pahali pa kukaa.
Katanga alipatikana na makosa ya kupanga shambulio katika vijiji na kwa mauaji ya raia wengi vijiji vilivyo kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2003.
Sasa ataachiliwa huru Januari 18, 2016.
No comments:
Post a Comment