Wednesday, November 18, 2015

Rufaa ya Blatter na Platini yakataliwa


Image captionSepp Blatter na Michel Platini
Maombi ya rais wa FIFA Sepp Blatter na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michel Platini ya kupinga kusimamishwa kazi kwa siku 90 waliowekewa na kamati ya Fifa yamekataliwa.
Wawili hao walisimamishwa kazi mnamo mwezi Octoba huku kamati ya Fifa ikichunguza madai ya ufisadi dhidi yao.
Blatter mwenye umri wa miaka 79,anatuhumiwa kutia saini kandarasi isio na manufaa yoyote kwa Fifa mbali na kufanya malipo yasio ya haki kwa Platini.
Wote wawili walikana kufanya makosa yoyote na watakata rufaa kwa mahakama ya usuluhishi.
Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke pia alisimamishwa kazi mnamo mwezi Oktoba lakini hakutajwa katika taarifa ya Fifa ya siku ya Jumatano.
Kamati hiyo ya Fifa inatarajiwa kufanya kikao kuhusu mashtaka hayo kabla ya krisimasi.

No comments:

Post a Comment