Sikukuu ya Uhuru na usafi, Mawaziri wamtesa Rais Magufuli, Mashamba, Viwanda kunyang’anywa?
Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye kuperuzi na kudadis redioni.
Rais Dk. John Magufuli afuta Sherehe za Uhuru zinazofanyika tarehe 9 December
kila mwaka, azuia gwaride litakalofanyika siku hiyo badala yake aokoa
mabilioni ya pesa ili zitumike kutatua matatizo mengine, aagiza siku
hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu
nchini.
Mchakato wa kunyang’anya mashamba na
viwanda kutoka kwa wamiliki walioshindwa kutekeleza masharti waliopewa
na Serikali umeanza, miongoni wa mashamba na viwanda hivyo ni kutoka
mikoa ya Morogoro, Lindi, Arusha, Mbeya, Morogoro, Tanga, Mwanza, Kilimanjaro na Dar es salaam, wamiliki ambao mpaka sasa hawajaendeleza mashamba waliopewa waagizwa kuyarudisha ndani ya siku 30.
Mawaziri wapya wamuweka Rais Dk. John Magufuli Dodoma akichambua majina ya makada watakaounda Baraza dogo la Mawaziri kwa ajili ya Serikali yake… Ndungu wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo wamefungua kesi Makama Kuu Mwanza kuiomba iondoe zuio la Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo kukatazwa kuaga mwili wa mtoto wao.
Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar yataendelea kufanyika leo Ikulu mjini Zanzibar, mazungumzo ya kikao hicho yataongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Kusikiliza Uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast bonyeza play hapa chini kwenye hii sauti.
No comments:
Post a Comment