Jasusi wa Marekani aliyeisaidia Israel aachiliwa
Afisa wa ujasusi wa
Marekani aliyehukumiwa kwa kupatikana na hatia ya kufanyia ujasusi
Israel ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka
30.
Jonathan Pollard, aliyekuwa wakati mmoja afisa wa maswala ya
usalama katika jeshi la wanamaji la Marekani alipatikana akiuzia maafisa
wa Israel nyaraka za siri za Marekani mwaka 1985.
Chini ya masharti ya kauchiliwa kwake, hapaswi kuondoka Marekani kwa muda wa miaka mitano baada ya kuachiliwa.
Viongozi wa Israel wamekuwa wakifanya kila juhudi kuishinikiza serikali ya Marekani kumwachilia Pollard kutoka gerezani.
No comments:
Post a Comment