Tuesday, November 24, 2015

Adele aweka wazi sababu ya kutamani kufanya ‘remix’ ya Hotline Bling na Drake!


Kati ya kazi za Drake ambazo zimetokea kupendwa na watu wengi sana ni latest single yake Hotline Bling, wimbo ambao wasanii wengi wamejitokeza kufanya cover song ya wimbo huo kwa miondoko tofauti… lakini itakuaje pale abampo Adele na Drake wataamua kufanya remix ya wimbo huo pamoja?
drizzyAdele
Kama wewe ni shabiki wa Adele na Drake basi ipokee hii mtu wangu, kwenye interview aliyofanya hivi karibuni na Danielle Graham, Adele ameweka wazi kwanini angependa kufanya remix ya wimbo huo na Drake mwenyewe…
>>> “Natamani kweli tufanye official remix… nampenda Drake, nampenda sana Drake, nimeenda hadi kutafuta koti alilolivaa kwenye video yake…. ni juzi tu hapa nimetoka kulipokea, niliagiza lile koti jekundu…” <<< Adele.
drizzyAdele3
Kingine ambacho inawezekana kimekufikia ama haijakufikia ni kwamba, Adele ana video yake binafsi aliyorekodi akicheza wimbo  huo lakini hajawahi kumuonyesha mtu na aliwaambia mashabiki wake wasitegemee kuiona video hiyo time yoyote ile…
>>> “Nadhani ilikuwa wiki tatu zilizopita nilipata vinywaji na mabestie zangu, tuliamua tutokee kusherekea mafanikio ya wimbo wangu wa ‘Hello’ sasa nikazidiwa vinjwaji (maana nilikuwa sijanywa pombe siku nyingi) nikajikuta nipo juu ya meza nacheza wimbo huo, na marafiki zangu wakaona wanirekodi… ” <<< alisema Adele huku akicheka sana.
drizzzyAdele2
Wimbo wa ‘Hello’ wa Adele unaendelea kushika kasi kwenye chati mbalimbali za muziki huku akishikilia nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard, Marekani, nafasi ambayo ilikuwa imeshikiliwa na Drake kwa wiki kadhaa kabla ya Hello kuweka headlines.

No comments:

Post a Comment