Papa Francis aonya kuhusu ongezeko la joto
Papa Francis
amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu
ya namna ya kupambana na ongezeko la joto duniani.
Akizungumza
katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
mazingira (UNEP) mjini Nairobi, Alhamisi kiongozi huyo wa Kanisa
katoliki duniani alisema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa
kutawala badala ya manufaa ya wote.
Kabla ya kuzungumzia hayo Papa
Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa
mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya
waumini katika mji mkuu wa Kenya.
Katika ziara yake barani
Afrika, kiongozi mkuu huyo wa Kanisa Katoliki amepangiwa kuelekea nchini
Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati Novemba 30.
No comments:
Post a Comment