Monday, November 9, 2015

Urusi yaiuzia Iran silaha kali ya ulinzi wa angani

Urusi yaiuzia Iran silaha kali ya ulinzi wa angani
Iran imenunua silaha kali ya ulinzi dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi.
Mtambo huo wa S-300 unauwezo mkubwa sana na yanaweza kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300.


Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya makubaliano haya na Iran.
Mwaka wa 2007 mataifa hayo yalikubaliana kuhusiana na mitambo hiyo ya ulinzi wa anga ila wakasitisha utekelezaji wake kufuatia marufuku iliyowekewa Iran kufuatia mipango yake ya kumiliki silaha za kinyuklia.
 
 
 
 
  
 
 Mtambo huo wa S-300 unauwezo mkubwa sana na yanaweza kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300.
Lakini punde baada ya kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha Iran sasa inapania kukamilisha mkataba huo.
Mtambo huo wa S-300 ulitumika kwa mara ya kwanza wakati wa vita baridi na ulionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kukabili ndege zaidi ya moja na makombora umbali wa kilomita 300.
Mkurugenzi wa kampuni inayotengeneza silaha hiyo , Rostec,bwana Sergei Chemezov aliwaambia waandishi wa habari wa RIA kuwa kandarasi hiyo imeshatiwa sahihi.

No comments:

Post a Comment