Thursday, December 31, 2015

COMING SOON LIVE INTERVIEW NA STEVEN KUTOKA CHUO CHA UKUTUBI NA UHIFADHI WA NYARAKA KIJANA AMBAYE HANA UWEZO WA KUONA (BLIND).



LAKINI ANAWEZA KUFANYA MABO YAKE KAMA KAWAIDA, KAMA KUINGIA DARASANI NA KUSOMA, KUTAMBUA RANGI MBALILIMBALI NA MENGINE MENGI, endelea kuwa karibu na TING MUGOA ili kuiona video hiyo soon kupitia facebook, instagram, na kupitia BLOG YETU WWW.TINGMUGOA.BLOGSPOT.COM na kupitina youtube ni TING MUGOA.

Image result for FACEBOOK
Maafisa nchini Misri wameufunga mtandao wa mawasiliano ya kijamii wa Facebook, ambao unawaunganisha zaidi ya watu milioni tatu. Wizara ya mawasiliano ya simu imesema kufungwa kwa mtandao huo hakuhusiani na sababu za kiusalama. Lakini baadhi ya wakosoaji wamesema mtandao huo umefungwa wiki chache tu kabla ya kutimia miaka mitano tangu lilipozuka vuguvugu la mapinduzi ya umma katika mataifa ya Kiarabu, ambalo lilisababisha kuondolewa madarakani Rais Hosni Mubarak. Majukwaa ya mawasiliano ya mitandao ya kijamii yalionekana kama chombo muhimu wakati wa vuguvugu la mwaka 2011 na ilifungwa mara moja, wakati maandamano ya umma kuipinga serikali ya Mubarak yakipamba moto. Majukwaa hayo yalitumika kuandaa maandamano na kueneza ukosoaji dhidi ya serikali.

Kiasi cha watu 16 wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa na miripuko iliyotokea jana kwenye migahawa mitatu kaskazini mashariki mwa Syria. Mkurugenzi wa shirika linalofatilia haki za binaadamu lenye makao yake Uingereza, Rami Abdel Rahman, amesema mripuko mmoja uliotokea kwenye mji wa Qamishli, ulisababishwa na mripuaji aliyejitoa muhanga. Shirika la habari la Amaq linalowaunga mkono wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu-IS, limesema kundi hilo limedai kuhusika na mashambulizi kwenye mji huo, ambao uko karibu na mpaka wa Uturuki na karibu na Iraq. Mji wa Qamishli uko chini ya udhibiti wa pamoja wa serikali ya Syria na uongozi wa Kikurdi, ambao wametangaza maeneo ya ''uhuru wa kujitawala'' kuzunguka maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Syria. Kwa mujibu wa shirika hilo, miripuko yote katika migahawa mitatu imetokea kwenye eneo linalodhibitiwa na vikosi vya serikali.

Wednesday, December 30, 2015


Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema serikali yake iko tayari kuzungumza na wanamgambo wenye itikadi kali wa Boko Haram ili kuwaachia huru wanafunzi wa kike 209 waliowateka nyara mwezi Aprili 2014 kwenye mji wa Chibok. Hata hivyo, Buhari amesema lazima kwanza Boko Haram wautambulishe uongozi wa kuaminika kwa ajili ya mazungumzo hayo. Majaribio mengine yalishindikana katika utawala uliopita kwa sababu maafisa walikuwa wanazungumza na watu wasio sahihi. Buhari amesema hakuna taarifa madhubuti za kijasusi kuhusu mahali waliko wasichana hao, wala namna afya zao zilivyo na hivyo mazungumzo hayo yanaweza yakaanza tu iwapo maafisa wa Nigeria watathibitisha kuwa wasichana hao wako hai. Mamia ya watu wanaoshikiliwa mateka na Boko Haram, waliachiwa huru katika miezi ya hivi karibuni, lakini hakuna msichana hata mmoja kutoka shule ya Chibok, ambaye alikuwa miongoni mwa walioachiwa huru.

Serikali nchini Ubelgiji imefuta sherehe na shamrashamra za Mwaka Mpya pamoja na ufyatuaji wa fataki kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Brussels, baada ya kugundulika njama ya wanamgambo wa itikadi kali kutaka kufanya mashambulizi wakati wa sikukuu hiyo. Meya wa Brussels, Yvan Mayeuer, amesema kwa bahati mbaya wamelazimika kufuta sherehe hizo zilizopangwa kufanyika leo usiku. Mji wa Brussels wenye wakaazi milioni 1.2 umekuwa katika hali ya tahadhari tangu Ufaransa iliposema watu kadhaa waliohusika na mashambulizi ya kigaidi ya Paris, Novemba 13, wanaishi mjini Brussels, ambako ni makao makuu ya Umoja wa Ulaya na Jumuia ya Kujihami ya NATO. Siku ya Jumanne polisi walisema wamewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya mjini Brussels. Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amesema uamuzi wa kufutwa sherehe za Mwaka Mpya ulikuwa mgumu, lakini ulio sahihi.

Umoja  wa  Afrika  leo  umetishia  kuyawekea vikwazo makundi  hasimu  nchini  Burundi  iwapo  yatashindwa kuhudhuria  mazungumzo  ya  amani  mwezi  ujao, wakati ukiibana  serikali   kukubali jeshi  la  kulinda  amani.
Serikali  ya  Burundi  na  upinzani, pande  zilizokutana nchini  Uganda  siku  ya  Jumatatu,  zinatarajiwa  kukutana tena  Januari  katika  mji  wa  kaskazini  mwa  Tanzania  wa Arusha kwa  mazungumzo  yenye  lengo  la  kumaliza miezi  kadhaa  ya  ghasia.
Ghasi  hizo  zimeongeza  hofu  ya  kurejewa  kwa  vita kamili  katika  taifa  hilo  dogo  la  Afrika  ya  kati, miaka tisa baada  ya  kumalizika  kwa  vita  vya  wenyewe  kwa wenyewe. Maafisa  wa  Uganda  wamesema  mazungumzo yataanza  tena  Januari  6  lakini  ujumbe  wa  serikali  ya Burundi  umesema  hakuna  muafaka  uliofikiwa  kuhusiana na  tarehe  ya  mkutano  huo.
Rais  wa  halmashauri  ya  Umoja  wa  Afrika  Nkosazana Dlamini-Zuma ameonya  kuhusu  vikwazo  hivyo  iwapo ghasia  zitaendelea  na  mazungumzo hayatafanyika.

Waziri  mkuu  wa  Iraq Haider al-Abadi  jana  alifanya  ziara katika  mji  uliokombolewa  wa  Ramadi, baada  ya  majeshi ya  serikali  kutangaza  kuukomboa  mji  huo  kutoka  kwa kundi  la  Dola  la  Kiislamu, na  kupata  ushindi  muhimu.
Abadi  aliwasili  kwa  helikopta  katika  mji  huo  ulioharibiwa kwa  vita, ambao  uko  kilometa 100 magharibi  ya  mji mkuu  Baghdad  na  ni  mji  mkuu  wa  jimbo  la  Anbar.
Waziri  mkuu ameapa  siku  ya  Jumatatu , baada  ya majeshi  yanayopambana  na  magaidi  kupandisha bendera  ya  taifa  katika  majengo  ya  serikali  mjini Ramadi kwamba atawaondoa  wanamgambo  wa  IS kutoka  nchi  hiyo  ifikapo mwishoni  mwa  mwaka  2016.
Ni  jambo  la  kawaida  kwa  waziri  mkuu  kutembelea  miji iliyokombolewa  lakini  amefurahishwa  mno na  ushindi katika  mji  wa  Ramadi, mji  ambao  majeshi  ya  serikali yaliupoteza  Mei mwaka  huu.
Image result for IS
Marekani  imesema  kiongozi wa  Dola  la  Kiislamu Mfaransa , ambaye  alihusika  katika  mashambulizi  ya mjini  Paris, ameuwawa  katika  mashambulizi  ya  anga  ya muungano  unaoongozwa  na  Marekani.
Charaffe al-Mouadan, ambaye  aliwasiliana  na  aliyedaiwa kuwa  kiongozi  wa  mauaji  katika  mji  mkuu  wa  Ufaransa Paris, ameuwawa  wakati  wa  shambulio  la  anga Desemba  24  mwaka  huu.
Wizara  ya  ulinzi  ya  Marekani  imesema  alikuwa  mmoja wa  viongozi 10  wa  juu  wa  IS waliouwawa  katika  muda wa miezi  michache iliyopita kwa  mashambulizi  ya  ndege zisizokuwa  na  rubani.

Msaidizi mkuu wa Kim Jong-un afariki


KimImage copyrightGetty
Image captionKim Yang-gon alihusika na uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Kusini
Msaidizi mkuu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amefariki katika ajali ya barabarani, shirika la habari la serikali la KCNA amesema.
Kim Yang-gon, 73, alikuwa katibu wa chama tawala cha Wafanyakazi na alisimamia uhusiano na Korea Kusini.
Alikuwa kwenye ujumbe wa ngazi za juu kutoka Korea Kaskazini uliosaidia kupunguza uhasama kati ya Pyongyang na Korea Kusini mwezi Agosti, baada ya majeshi ya nchi hizo mbili kufyatuliana makombora.
Shirika la habari la KCNA lilimweleza kama rafiki mkuu wa Kim Jogn-un na mshirika mkuu wa mapinduzi.
Kim
Image captionKim Yang-gon alikuwa katibu wa chama tawala
"Rafiki Kim Yang-gon, katibu wa Chama cha Wafanyakazi na mwanachama wa kamati kuu ya Politbureau... alifariki katika ajali ya barabarani saa thenashara na robo asubuhi, Jumanne, akiwa na umri wa miaka 73," KCNA ilisema, bila kutoa habari zaidi.
Shirika hilo limeongeza kuwa Kim Jong-un atahudhuria mazishi ya kiongozi huyo pamoja na maafisa 80 wakuu wa serikali.

Wachimba migodi wapatikana hai China




Wachimba migodi wanane waliokwama ardhini kwa siku tano huko China wamepatikana wakiwa hai.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa makundi ya waokoaji bado hawajafanikiwa kuwaondoa chini ya ardhi ila wamewasiliana nao na kutuma vifaa na vyakula.
Wachimba migodi hao waliwaambia waokoaji kuwa walikuwa wamekwama katika njia za chini kwa chini.
Waokoaji ambao walikuwa wametupa camera ardhini walifurahia kuwapata hai wachimba migodi hao.
Wakati huohuo mkasa wa awali wa kuporomoka kwa timbo la mawe na vifusi vya ujenzi ulisajiliwa na vipimo vya tetemeko ya ardhi.
Wachimba migodi tisa bado hawajulikani waliko.
Saba waliokolewa mapema na moja anafahamika kuaga dunia.

I
Mawe yaliporoka kwenye mgodi huo ulio mkoa wa mashariki wa Shandong.
Ripoti zinasema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea mmiliki wa mgodi huo alijiua wa kujirusha ndani ya kisima.
China inahistoria ndefu ya mikasa ya timbo na migodi inayolaumiwa kwa utepetevu wa idara za serikali kuhakikisha sheria na kanuni za afya na usalama zinazingatiwa na kutekelezwa na wamiliki wa migodi.

Uchaguzi wa urais waanza Afrika ya Kati


Uchaguzi

Image copyrightAFP
Image caption
Uchaguzi huu umeahirishwa mara nne mwaka huu

Raia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanapiga kura leo katika uchaguzi wa urais na ubunge ambao unalenga kurejesha uthabiti nchini humo.
Wagombea 30 wanawania urais katika uchaguzi huo ulioahirishwa mara kadha.
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa wanatumai kuzuia marudio ya ghasia zilizokumba kura ya maamuzi kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huu wiki tatu zilizopita.
CAR imeathiriwa pakubwa na mapigano tangu wapiganaji wa Kiislamu wa Seleka wachukue mamlaka Machi 2013.
Wapiganaji wa Kikristo waliojulikana kama anti-Balaka baadaye walivhukus silaha na kuanza kupigana na wa Seleka.
Januari 2014, serikali ya mpindo iliundwa ikiongozwa na kaimu rais Catherine Samba-Panza.
Uchaguzi mkuu nchini humo umeahirishwa mara kadha tangu Februari 2015 kutokana na machafuko na kuchelewa kwa maandalizi ya uchaguzi.
Wagombea watatu ndio wanaoaminika kuwa na ushawishi mkubwa.
Wawili kati yao, Martin Ziguele na Anicet Dologuele, waliwahi kuhudumu kama mawaziri wakuu chini ya rais wa zamani marehemu Ange-Felix Patasse.
Wa tatu, Karim Meckassoua, ni Mwislamu aliyehudumu kama waziri chini ya Rais Francois Bozize hadi walipoondolewa mamlakani na wapiganaji wa Seleka mwaka 2013.

CARImage copyrightAFP
Image caption
CAR ni moja ya nchi alizozuru Papa Francis kwenye ziara yake ya kwanza Afrika Novemba

Wachunguzi wanasema huenda kukafanyika duru ya pili ya uchaguzi, sana mwishoni mwa Januari.
Uchaguzi pia unafanyika kuchagua wabunge 105.
Baada ya kuchukua uongozi, waasi wa Seleka walimuweka uongozini Michel Djotodia, akiwa kiongozi wa kwanza Mwislamu katika taifa hilo lenye Wakristo wengi.
Lakini baada ya shinikizo kutoka kwa viongozi wa kanda na mkoloni wa zamani Ufaransa, Bw Djotodia aling’atuka na nafasi yake ikachukuliwa na Bi Samba-Panza.
Bw Djotodia na Bw Bozize wote wamo uhamishoni na wamewekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa na Marekani kwa kuchangia machafuko nchini humo.

Saturday, December 26, 2015

Tetemeko la ardhi lakumba Afghanistan


PeshawarImage copyrightEPA
Image captionWatu 17 wamejeruhiwa mjini Peshawar, Pakistan
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.3 limekumba maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan, na kuathiri maeneo ya mbali hadi India.
Kwa mujibu wa Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa mkoa wa Badakhshan, karibu na mpaka wa Pakistan na Tajik.
Haijabainika iwapo kulikuwa na majeruhi eneo hilo, lakini watu 17 walijeruhiwa katika mji wa Peshawar, nchini Pakistan.
Mamia ya watu waliuawa eneo lilo hilo 26 Oktoba baada ya tetemeko jingine la ardhi kutokea.
Eneo hilo limekuwa likikumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi inayosababishwa na mgongano wa maeneo bara ya India na Eurasia.
Maeneo hayo yanaingiliana kwa kiwango cha sentimeta 4-5 kila mwaka.
Mwaka 2005, tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.6 kwenye vipimo vya Richter katika eneo la Kashmir, linalotawaliwa na Pakistan, liliua watu zaidi ya 75,000
Na Aprili mwaka huu, Nepal ilikumbwa na tetemeko mbaya zaidi nchini humo lililoua watu 9,000 na kuharibu nyumba 900,000.

Ukumbi wa Waislamu wavamiwa Corsica


AjaccioImage copyrightAFP
Image captionUkumbi wa maombi uliharibiwa mjini Ajaccio
Kundi la watu limevamia na kuharibu ukumbi wa maombi wa Waislamu katika kisiwa cha Ufaransa cha Corsica katika kinachoonekana kuwa shambulio la kulipiza kisasi kushambuliwa kwa wazima moto kisiwani humo.
Maafisa wa serikali wanasema kundi ndogo la waandamanaji pia lilijaribu kuteketeza Koran katika mji mkuu wa kisiwa hicho Ajaccio.
Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika katika mji huo mkuu kulalamikia kujeruhiwa kwa wazima moto wawili na afisa mmoja wa polisi Alhamisi.
Watatu hao walishambuliwa na vijana waliokuwa wamejifunika nyuso.
Serikali imeshutumu visa vyote viwili na kuahidi kuadhibu waliohusika.
Shirika la habari la AFP linasema baadhi ya waandamanaji walienda hadi eneo ambapo maafisa hao walishambuliwa na kuanza kuimba “Waarabu waondoke!” na “Hapa ni nyumbani.”
Baadaye, walishambulia ukumbi wa maombi wa Waislamu, wakapora na kuchoma kiasi baadhi ya vitabu, zikiwemo nakala za Koran.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ametaja shambulio hilo kuwa “lisilokubalika”.
Baraza la Waislamu la Ufaransa pia limeshutumu ghasia hizo.
Ufaransa imeimarisha usalama wakati huu wa sikukuu ya Krismasi baada ya shambulio la 13 Novemba kusababisha vifo vya watu 130.

Kiongozi wa kundi la waasi auawa Syria


JayshImage copyrightAFP
Image captionAlloush ndiye aliyeanzisha kundi la Jaysh al-Islam
Kiongozi mkuu wa kundi la waasi la Jaysh al-Islam, moja ya makundi yenye nguvu zaidi Syria, ameuawa kwenye shambulio la makombora.
Zahroun Alloush, 44, ambaye ndiye mwanzilishi wa kundi hilo aliuawa kwenye shambulio la makombora mashariki mwa Damascus alipokuwa kwenye mkutano.
Aliuawa pamoja na viongozi wengine wa kundi hilo, habari ambazo zimethibitishwa na makundi ya waasi na jeshi la Syria.
UrusiImage copyrightGetty
Image captionUrusi na Syria zilikataa kutambua mkutano huo wa waasi Saudi Arabia
Kundi hilo linaloungwa mkono na Saudi Arabia ni moja ya makundi makubwa ya waasi wanaopigana na Rais Bashar Assad na ngome yake ni maeneo ya Ghouta, mashariki mwa nchi hiyo.
Majuzi lilihudhuria mkutano mkuu wa wapinzani wa Bw Assad mjini Riyadh, mkutano ambao ulijadili mkakati wa mazungumzo ya Amani na serikali.
Makombora kumi yanadaiwa kuanguka eneo ambalo makamanda wa Jaysh al-Islam walikuwa mkutanoni, kwa mujibu wa runinga ya al-Arabiya inayofadhiliwa na serikali ya Saudi Arabia.
Naibu kiongozi wa kundi hilo pia aliuawa.
JayshImage copyrightReuters
Image captionKundi la Jaysh al-Islam limekuwa likipigana katika mji wa Damascus
Jaysh al-Islam baadaye walimteua Issam al-Buwaydani – ajulikanaye pia kama Abu Humam – kuwa kiongozi wake mpya.
Bw al-Buwaydani anatoka mji wa Douma, mashariki mwa Damascus.
Jeshi la Syria, kupitia taarifa kwenye runinga ya taifa, limesema ndilo lililotekeleza shambulio hilo lakini baadhi ya wanaharakati wanasema lilitekelezwa na Urusi.
Duru nyingine zimedokeza huenda jeshi la Syria lilitekeleza shambulio hilo likitumia makombora ya Urusi.
Urusi, ambayo ni mshirika mkuu wa Rais Assad, imekuwa ikitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya wapinzani wa Bw Assad tangu mwisho wa Septemba.