Sunday, December 20, 2015


Utafiti: Hakuna ugaidi wa kadri au wenye misimamo mikali


Image copyrightAP
Image captionUtafiti: Hakuna ugaidi wa kadri au wenye misimamo mikali
Thuluthi moja ya wapiganaji nchini Syria takriban wapiganaji laki moja wanaiunga mkono kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.
Utafiti mpya umebaini kuwa hata kundi la
IS likipigwa na kushindwa huo hautakuwa ndio mwisho wa ugaidi duniani.
Utafiti huo uliofanywa na shirika la The Centre on Religion and Geopolitics linalohusiana na aliyekuwa waziri wa Uingereza Tony Blair unasema kuwa makundi 16 ya waasi nchini Syria yako tayari kuchukua mahala pa kundi la wanamgambo wa Islamic State, ikiwa majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani yatalishinda.
Ripoti iliyotolewa na kituo cha kidini na maswala ya kutathmini siasa katika Mashariki ya Kati, ambacho kinahusishwa na aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, pia kinasema kwamba asilimia 60% ya waasi wanajumuishwa kama wapiganaji wa kiislamu.
Takriban watu 250,000 wameuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria .
Image copyrightIslamic State
Image captionTakriban watu 250,000 wameuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria .
Mamilioni zaidi ya watu wamelazimika kutoroka makwao.
Tangu mwezi Septemba, ndege za kijeshi za Urusi zimekuwa zikiishambulia Syria.
Hii ni kuongezea kwa mwaka mmoja wa mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani.
Ripoti hiyo inahoji uwezo wa mataifa ya kigeni kutofautisha kati ya wapiganaji wenye msimamo wa kadri au wale wenye misimamo mikali, ni finyu mno kwa sababu kuna miungano mingi tofauti nchini humo.

No comments:

Post a Comment