Umoja wa Afrika watishia kuiwekea vikwazo Burundi.
Umoja wa Afrika leo umetishia kuyawekea vikwazo makundi hasimu nchini Burundi iwapo yatashindwa kuhudhuria mazungumzo ya amani mwezi ujao, wakati ukiibana serikali kukubali jeshi la kulinda amani.
Serikali ya Burundi na upinzani, pande zilizokutana nchini Uganda siku ya Jumatatu, zinatarajiwa kukutana tena Januari katika mji wa kaskazini mwa Tanzania wa Arusha kwa mazungumzo yenye lengo la kumaliza miezi kadhaa ya ghasia.
Ghasi hizo zimeongeza hofu ya kurejewa kwa vita kamili katika taifa hilo dogo la Afrika ya kati, miaka tisa baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maafisa wa Uganda wamesema mazungumzo yataanza tena Januari 6 lakini ujumbe wa serikali ya Burundi umesema hakuna muafaka uliofikiwa kuhusiana na tarehe ya mkutano huo.
Rais wa halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ameonya kuhusu vikwazo hivyo iwapo ghasia zitaendelea na mazungumzo hayatafanyika.
No comments:
Post a Comment