Gazeti latangaza kifo cha Father Christmas
Gazeti moja nchini Norway limelazimika kuomba radhi baada ya kuchapisha tangazo la kicho cha "Father Christmas".
Tangazo
hilo lilikuwa la "Mpendwa Father Christmas, aliyezaliwa 12 Desemba
1788", ambaye alidaiwa kufariki tarehe 3 Desemba mjini Nordkapp, ulio
kaskazini mwa Norway.Ibada ya mazishi ilifaa ifanyike 28 Desemba katika kanisa la North Pole Chapel", kwa mujibu wa tangazo hilo.
Gazeti hilo la Aftenposten, ambalo ndilo la pili kwa umaarufu nchini Norway, lilisema kosa hilo lilitokana na taratibu zake za utenda kazi.
"Aftenposten ina taratibu kali kuhusu habari na kutumiwa kwa ishara na mifano katika matangazo yetu ya vifo. Tangazo hili linakiuka taratibu hizi na halikufaa kuchapishwa,” gazeti hilo limesela kupitia taarifa.
“Tutachunguza kubaini kilichosababisha hili,” imeongeza taarifa hiyo.
Gazeti hilo limesema limeondoa tangazo hilo kutoka kwa tovuti yake baada ya kufahamishwa kuhusu kosa hilo.
No comments:
Post a Comment