Friday, December 18, 2015

Islamic State yabanwa kupata fedha


Image copyrightAP
Image captionWapiganaji wa Islamic State
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kukata mifumo ya fedha kwa kundi la Islamic State.
Mkutano wa kwanza wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa mawaziri wa fedha umeafiki juu ya azimio hilo lililobuniwa kwa ajili ya kuzuia fedha kuwafikia wanamgambo wa Islamic State.
Mkutano huo umeyataka mataifa kufanya juhudi za haraka kukata mifumo ya udhamini wa fedha kwa kundi hilo kwa kuzuia wizi wake wa mafuta na raslimali nyingine.

No comments:

Post a Comment