Wednesday, December 16, 2015

Filamu mpya ya Star Wars yazinduliwa


London
Filamu mpya ya mwendelezo wa filamu za Stars Wars, iliyosubiriwa kwa hamu sana, imeonyeshwa kwa mara ya kwanza Los Angeles.
Filamu hiyo ya Star Wars: The Force Awakens, imeshirikisha waigizaji kutoka kwa filamu ya kwanza kabisa Harrison Ford, Mark Hamill na Carrie Fisher na wageni wakiwemo John Boyega na Daisy Ridley.
Yaliyomo ndani yamewekwa kama siri kuu na wanahabari wametakiwa kutotoa tathmini kuihusu hadi Jumatano.
Lakini baadhi ya watu tayari wametoa tathmini ya filamu hiyo baada ya kuitazama na wanasema ni filamu nzuri.

No comments:

Post a Comment