Waziri mkuu wa Iraq atembelea Ramadi.
Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi jana alifanya ziara katika mji uliokombolewa wa Ramadi, baada ya majeshi ya serikali kutangaza kuukomboa mji huo kutoka kwa kundi la Dola la Kiislamu, na kupata ushindi muhimu.
Abadi aliwasili kwa helikopta katika mji huo ulioharibiwa kwa vita, ambao uko kilometa 100 magharibi ya mji mkuu Baghdad na ni mji mkuu wa jimbo la Anbar.
Waziri mkuu ameapa siku ya Jumatatu , baada ya majeshi yanayopambana na magaidi kupandisha bendera ya taifa katika majengo ya serikali mjini Ramadi kwamba atawaondoa wanamgambo wa IS kutoka nchi hiyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2016.
Ni jambo la kawaida kwa waziri mkuu kutembelea miji iliyokombolewa lakini amefurahishwa mno na ushindi katika mji wa Ramadi, mji ambao majeshi ya serikali yaliupoteza Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment