Tuesday, December 15, 2015

NDEGE ZATEREKEZWA AIR PORT, MWENYE NAZO HAJULIKANI.

Eti ndege zimetelekezwa na mwenyewe hafahamiki ??!! Kichwa cha habari huenda kikakushtua lakini ndio hivyo, na ndege zenyewe zimekaa airport mwaka mzima uwanja wa Kuala Lumpur, Malaysia.
Baada ya ndege hizo kutekelezwa uwanjani hapo kwa zaidi ya mwaka mmoja, ilibidi uongozi wa uwanja huo wapeleke matangazo magazetini kutaarifu kwamba kwa mmiliki wa ndege hizo ajitokeze kutoa ndege zake ndani ya siku 14, kama asipotokea basi ndege hizo zinauzwa !!
Hizi ni sehemu ya ndege hizo tatu zilizotelekezwa.
Hizo ni sehemu ya ndege hizo tatu zilizotelekezwa.
Baada ya tangazo hilo kutoka magazetini December 09 2015 na kuchukua headlines mitandaoni, taarifa nyingine iliyonifikia na kuripotiwa na mtandao wa Daily Mail ni kwamba Kampuni ya Swift Air Cargo imejitokeza na kusema wao ndio wamiliki wa ndege hizo tatu kubwa za mizigo…
SWIFT
Hili ndio tangazo la ndege hizo gazetini.

No comments:

Post a Comment