Polisi apatikana na hatia ya ubakaji Oklahoma
Afisa mmoja wa
polisi mjini Oklahoma amepatikana na hatia ya ubakaji pamoja na
kumnyanyasa mwanamke mmoja mweusi katika eneo la umasikini alilokuwa
akifanya kazi.
Daniel Holtzclaw mwenye umri wa miaka 29
aliwasimamisha wanawake hao akiwa katika doria za kikazi, kabla ya
kuwapekua na baadaye kuanza kuwanyanyasa.
Holtzclaw alipatikana na
hatia ya kuwanyanyasa waathiriwa wanane ikiwemo bibi mmoja aliye katika
miaka yake ya hamsini pamoja na msichana mmoja wa miaka 17.
Baraza la waamuzi lilipendekeza hukumu ya miaka 263.
Anatarajiwa kuhukumiwa mnamo mwezi Januari.
''Haki imetendeka leo na muhalifu aliyevaa sare anaelekea jela'',wakili wa kaunti ya Oklahoma David Prater alisema.
Hukumu
hiyo ilitolewa katika siku ya kuzaliwa ya Holtzclaw,ripota mmoja katika
kesi hiyo alituma kanda ya video ya wafuasi wa mwathiriwa katika
mtandao wa twitter wakiimba happy birthday baada ya hukumu hiyo
kutolewa.
No comments:
Post a Comment