Wednesday, December 30, 2015


Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema serikali yake iko tayari kuzungumza na wanamgambo wenye itikadi kali wa Boko Haram ili kuwaachia huru wanafunzi wa kike 209 waliowateka nyara mwezi Aprili 2014 kwenye mji wa Chibok. Hata hivyo, Buhari amesema lazima kwanza Boko Haram wautambulishe uongozi wa kuaminika kwa ajili ya mazungumzo hayo. Majaribio mengine yalishindikana katika utawala uliopita kwa sababu maafisa walikuwa wanazungumza na watu wasio sahihi. Buhari amesema hakuna taarifa madhubuti za kijasusi kuhusu mahali waliko wasichana hao, wala namna afya zao zilivyo na hivyo mazungumzo hayo yanaweza yakaanza tu iwapo maafisa wa Nigeria watathibitisha kuwa wasichana hao wako hai. Mamia ya watu wanaoshikiliwa mateka na Boko Haram, waliachiwa huru katika miezi ya hivi karibuni, lakini hakuna msichana hata mmoja kutoka shule ya Chibok, ambaye alikuwa miongoni mwa walioachiwa huru.

No comments:

Post a Comment