Colombia yahalalisha matumizi ya bangi
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametia saini sheria ya kuhalalisha matumizi,ukuzaji na uuzaji wa bangi kama dawa. Santos amesema kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi nchini humo hakutahujumu vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya bali itatoa fursa kwa utafiti wa kisayansi kuimarishwa kuhusu dawa hizo nchini Colombia. Rais huyo ameongeza lengo lao ni kuhakikisha wagonjwa wanaweza kupata dawa zinazotengezwa nchini humo ambazo ni salama, za viwango vya juu na zinazopatikana kwa urahisi. Wizara ya afya pia itatoa kibali cha kuuzwa nje kwa bangi kwa nchi ambazo hazijaharamisha matumzi yake.
No comments:
Post a Comment