Mother Teresa' kuwa mtakatifu
Makao Makuu ya Vatican yemedhibitisha kwamba mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na mtauwa; Marehemu 'Mother Teresa' atatangazwa mtakatifu.
Taarifa ya Vatican inasema Papa Francis ameridhia utaratibu wa kumtangaza mtakatifu mtauwa huyo baada ya kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kadhaa kwenye ubongo wake.
Vyombo vya habari vya Italia vinabashiri huenda sherehe ya kumtawaza mtauwa huyo kuwa mtakatifu ikafanyika mwezi Septemba mwaka ujao.
'Mother Teresa' alizapewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia masikini kwenye vitongoji wa jimbo la Kolkata nchini India. Alifariki dunia mwaka 1997.
No comments:
Post a Comment