Thursday, December 10, 2015

Marekani yazidi kuisambaratisha IS.




Maofisa wa polisi nchini Marekani wanaoshughulika na mapambano ya kuutokomeza ugaidi, wamesema mkuu wa masuala ya fedha wa kundi la kigaidi la Islamic State ameuawa kutokana na shambulio la anga karibu na mji wa Tal Afar nchini Iraq, katika wiki za hivi karibuni.
Mjumbe wa serikali ya Marekani katika vikosi vya muungano wa kimataifa dhidi ya IS, Brett McGurk, ametoa maelezo katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba Muwaffaq Mustafa Mohammed al-Karmoush ambaye anajulikana kama Abu Salah na maofisa wengine wawili wa ngazi za juu wa kundi la IS waliuawa katika oparesheni maalumu ya kuharibu miundombinu ya kifedha ya kundi hilo.
Ingawa mpaka sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na tukio hilo. Vikosi vya kijeshi vya Marekani na vile vya muungano wa majeshi washirika vimekuwa vikiendeleza mashambulizi ya anga dhidi ya wanajeshi wa IS nchini Iraq na Syria kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

No comments:

Post a Comment