Saturday, December 26, 2015

Rais amzuia mwanamume kujiua Uturuki


UturukiImage copyrightAP
Image captionMwanamume huyo alikuwa anatatizwa na msongo wa mawazo
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimshawishi mwanamume, aliyetaka kujiua kwa kujirusha kutoka kwa daraja, kubadilisha nia yake na kutojiua, afisi yake imesema.
Mwanamume huyo alikuwa amepanga juu ya uzio wa daraja la Bosphorus, linalounganisha Ulaya na bara Asia na alikuwa anatishia kujiua.
Msafara wa magari ya Bw Erdogan ulikuwa unapita kwenye daraja hilo mjini Istanbul wakati huo.
Picha zilizoonyeshwa kwenye televisheni zilionyesha wahudumu wa Bw Erdogan wakimsihi mwanamume huyo aliyekuwa akitokwa na machozi kuzungumza na rais.
Mwanamume huyo alitembea hadi kwenye gari la rais huyo na wakazungumza.
Image copyrightAP
Image captionErdogan alizungumza naye akiwa ndani ya gari lake, na akiwa ameweka simu kwenye sikio moja
Baada ya muda mfupi, alisindikizwa kutoka eneo hilo.
Mwanamume huyo alikuwa akitatizwa na msongo wa mawazo kutokana na matatizo ya kifamilia, na polisi walikuwa wamejaribu kumzuia asijirushe kwa saa mbili bila mafanikio, shirika la habari la Dogan limeripoti.
Afisa wa afisi ya rais huyo ameambia shirika la habari la Associated Press kwamba kiongozi huyo aliahidi kumsaidia.
UturukiImage copyrightJupitar grab
Image captionPolisi walikuwa wamejaribu kumshawishi aondoke bila mafanikio

No comments:

Post a Comment