Thursday, December 10, 2015

Wapinzani Syria wataka amani



Makundi ya upinzani nchini Syria wamekubaliana kuwa na tamko moja kwa serikali juu ya mazungumzo ya Amani yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.Waraka uliotengezwa umesainiwa baada ya mkutano wa siku mbili uliofanyika Saudi Arabia huku likiachana na matakwa ya awali ya kumtaka raisi Bashar Al Assad kujiuzulu kabla ya makubaliano yeyote.Mwenyekiti wa mkutano huo Abdulaziz Al-Sager ametoa maelezo ya kipi kitafuata baada ya mazungumzo hayo…
"Kutakuwa na mkutano ambao utaamuliwa na umoja wa mataifa hapo Januari,Utakua ni mkutano baina ya upinzani na serikali ya Syria kuweza kupita kipindi hiki cha mpito.Mkutano huu utachukua siku kumi za mwanzoni mwa Januari."
Lakini kwa upande wao upinzani wanasema Assad lazima atatoka wakati ambapo watakapotengeneza serikali mpya.Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Marekani ,John Kirbly ameyakaribisha maoni hayo na kusema ni hatua nzuri itakayoweza kumaliza migogoro ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Image copyrightNA
Image captionWilliam Hague akizungumzia namna ya kuwasaidia wapinzani Syria
"Hii ni hatua muhimu ambayo inaweza kuwaweka katika sehemu nzuri wakati wanapoanza majadiliano na serikali mwanzoni mwa mwezi januari.hii ni hatua muhimu ya kufika huko.Bado kuna kazi Zaidi kuanzia sasa ,hitimisho la mkutano wa leo na baadae mwanzoni mwa januari wakati ambapo tunategemea majadiliano haya ya kisiasa yataendelea .Kwa mfano jambo muhimu ni kutengeneza timu kubwa ya kujadilana."
Afisa mwandamizi katika hazina ya Marekani amesema kwamba wapiganaji wa Islamic State wamepora takriban dola bilioni moja za kimarekani katika mabenki yaliyopo katika maeneo wanayoyahodhi huko nchini Iraq na Syria.
Akiongea mjini London, afisa huyo amesema IS walipata zaidi dola milioni mia tano katika mauzo ya mafuta.
Ameongeza kusema, miongoni mwa wateja ni serikali ya rais Bashar al-Assad, ambayo wanataka kuitoa madarakani.

No comments:

Post a Comment