Tuesday, December 22, 2015


AMNESTY YAINYOOSHEA KIDOLE BURUNDI.



Image captionRaia wa Burundi wakiomboleza vifo vya jamaa zao

Shirika la kutetea haki za Binadamu Ulimwenguni la Amnesty International,limeituhumu serikali ya Burundi kwa mauaji watu wasio na hatia na matumizi mabaya ya jeshi la nchi hiyo.
Shirika hilo limelaani mauaji yaliyotokea Desemba 11 ambapo watu nane waliuawa wakati jeshi la serikali lilipokuwa likijihami dhidi ya mashambulizi ya waasi watatu waliovamia vituo vitatu tofauti vya jeshi.
Serikali ya Burundi iliwaelezea wale waliouawa kuwa ni maadui,jambo ambalo linapingwa vikali na Amnesty ambao wanasema kuwa wengi wa waliouawa ni watu wasio na hatia na raia wa taifa hilo.
Ripoti ya shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.

Image captionRipoti ya shirika hilo imeeleza kuwa wengine walichukuliwa nyumbani kwao na kuuawa kwa kupigwa risasi.

Kutokana na hali hiyo Umoja wa Afrika AU unasisitiza baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha mpango wake wa kupeleka kikosi cha wanajeshi 5000 wa kulinda amani nchini kufuatia mauaji ya raia
yanayoendelea.
Hata hivyo serikali ya Burundi inapinga hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment