Thursday, December 3, 2015

Kumbe Tundaman anatamani kuona wasanii hawa wakongwe warudi kwenye game !!


Jana December 2 2015, msanii wa Biongofleva Tundaman aliingia kwenye vichwa vya habari sehemu tofauti baada ya kutoa wimbo wake mpya unaitwa “Mama Kijacho“… Tundaman anasema kwamba sehemu ya wimbo huo ameandika kwa kutumia story alizopewa na mama yake jinsi alivyokua anasumbua wakati akiwa na ujauzito aliozaliwa Tundaman.
Zaidi ya hapo Tunda anasema anatamani kuwaona wasanii hawa wanarudi kwenye pick yao kama zamani kwa sababu anaamini uwezo wao kwenye sanaa ni mkubwa sana.
Chidi Benz
Bila Chidi Benz basi Tundaman asingetoka kama ilivyotoka kipindi kile, ngoma yangu ya ‘Neila’ Chid Benz alifanya kazi nzuri sana kwenye ile ngoma… Ukiachana na ile ngoma Chid Benz ni msanii mwenye historia kubwa kwenye Hiphop ya Tanzania nataka sana kumuona anarudi kwenye pick yake.”- Tundaman.
Z Anto
Kipaji kikubwa sana ambacho nimekua nae karibu wakati tupo Tip Top, ana uwezo wake wa kutunga ngoma ambazo sio rahisi watu wengine kuweza kuziimba lakini alikua anafanya hivyo na ku-hit.“– Tundaman.
Ferooz
Nahitaji kumuona huyu jamaa anarudi kwenye muziki tena kwa sababu naamini kwenye uandishi wake na jinsi anavyoimba kwa hisia. Inaweza kuwa ngoma ya ku-party au kuelimisha zote anaweza kuzifanya kwa hisia kali.”- Tundaman.

No comments:

Post a Comment