Sunday, December 20, 2015




Wananchi wa Uhispania leo wanapiga kura katika kile kinachotarajiwa kuwa moja ya chaguzi zenye ushindani mkubwa kuwahi kushudhuiwa katika historia ya hivi sasa. Baada ya siku 14 za kampeni, chama cha kihafidhina kilichoko madarakani cha Waziri Mkuu Mariano Rajoy kina matumaini ya kuchaguliwa tena, licha ya upinzani mkali siyo tu kutoka kwa mahasimu wao wa Kisoshalisti, lakini vyama viwili vipya kikiwemo cha mrengo wa kati cha Ciudadanos na kinachopinga sera za kubana matumizi cha Podemos, vinavyotaka mabadiliko. Utabiri wa maoni unaonyesha kuwa chama tawala cha Popular-PP kitashinda kwa sehemu kubwa ya kura, lakini bila ya kuwa na wingi wa kutosha kuunda serikali, hali itakayokilazimu kuungana na chama kingine cha kisiasa na kuunda serikali ya mseto.

No comments:

Post a Comment