Wizara ya ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa wanajeshi wake wametumwa katika jimbo la Helmand kusini mwa Afghanistan. Hatua hiyo inakuja baada ya wanamgambo wa Taliban kuyadhibiti maeneo makubwa ya jimbo hilo. Gazeti la Uingereza la The Times limeripoti miongoni mwa wanajeshi waliotumwa kwenda kupambana dhidi ya Taliban ni kikosi maalum cha wanajeshi 30 wa angani watakaoshirikiana na wanajeshi 60 wa Marekani walioko Afghanistan. Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Uingereza amesema wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya kujihami ya NATO ambacho kinatoa ushauri wa kijeshi kwa wanajeshi wa Afghanistan na hawatahusika moja kwa moja katika mapambano na Taliban.
No comments:
Post a Comment