Tuesday, December 8, 2015

Mtoto wa Kim na Kanye West aitwa Saint West


Kim


Kim Kardashian West na Kanye West wamempa mtoto wao wa pili jina Saint West.
Kim amethibitisha jina hilo kwenye tovuti yake, siku tatu baada ya kutangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume.
Binti wao, aliyepewa jina North West, alizaliwa Juni 2013.
Kim alitangaza kwamba alikuwa ameshika mimba mara ya pili kwenye kipindi chake cha runingani cha Keeping Up with the Kardashians mwishoni mwa mwezi Mei.
Alifichua kwamba mtoto wake wa pili angekuwa mvulana kwenye ujumbe aliomuandikia Kanye West kwenye Twitter siku ya kuwakumbuka kina baba duniani, yaani Father's Day.
Wawili hao hawajasema ni kwa nini wakachagua jina Saint West lakini baadhi ya ripoti zinasema ni kwa sababu Kim alisumbuka sana alipokuwa na mimba yake.
Image copyright
Jina la mtoto huyo limevuma sana kwenye Twitter muda mfupi baada ya kutangazwa, baadhi wakilifurahia.

No comments:

Post a Comment