Sunday, December 20, 2015


Ukuta kuadhibu waendao haja ndogo ovyo


HackneyImage copyrightPublicis Pixelpark
Image captionBaraza la Hackney limekuwa likitumia £100,000 kila mwaka kusafisha kuta
Aina mpya ya rangi ambayo imeundwa kwa mtindo maalum ili kurejesha mkojo kwa anayejaribu kuukojolea ukuta uliopakwa rangi hiyo, imeanza kujaribiwa na manispaa moja jijini London.
Rangi hiyo ya majimaji itakuwa ikipakwa katika maeneo maarufu kwa wanywaji pombe, katika tarafa za Shoreditch na Dalston, mashariki mwa London.
Manispaa ya Hackney, imesema imekuwa ikitumia £100,000 kusafisha mkojo kutoka katika kuta za manispaa hiyo na pembezoni mwa barabara, mahala ambapo watu huenda haja ndogo ovyo.
Feryal Dermici, ambaye ni mbunge wa manispaa hiyo anasema: "ikiwa hatua ya kuwapiga faini haiwazuii kukojoa ovyo barabarani na pembezoni mwa njia, sasa hatari ya kumwagikiwa na mkojo wao wenyewe, litakuwa jambo la busara".
Sasa, adhabu ni kujenga kizuizi itakayopakwa rangi ambayo itawezesha mkojo kumrudia mkojoaji, ili anapomwagikiwa na mkojo wake mwenyewe, basi atapata adhabu inayomfaa.
Pia lengo jingine ni kuzuia mkojo kulowesha ukuta, kuondoa madoadoa ya uchafu na uvundo.
Haijafichuliwa hasa maeneo ambayo itapakwa rangi hiyo, ili wanaoenda haja wasijue na kukwepa maeneo hayo pekee.

No comments:

Post a Comment