Thursday, December 3, 2015

Nigeria yaipunguzia faini kampuni ya MTN

Nigeria yaipunguzia faini kampuni ya MTN
Nigeria imepunguza faini kubwa ambayo ilikuwa imeipiga kaMpuni kubwa zaidI ya simu za mkononi barani Afrika hadi dola billioni tatu nukta nne.
Kampuni hiyo ya Afrika Kusini MTN ilipigwa faini mwezi Oktoba baada ya kushindwa kuzima kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa kutoka kwa mtandao wake.
Faini hiyo ilimlazimisha mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo kujiuzulu na mauzo ya hisa ya kampuni kudorora.
 
Faini hiyo ni zaidi ya faida ya mwaka mmoja ya MTN nchini Nigeria. 
Lakini kufuatia wiki kadhaa za majadiliano utawala umekubali kupunguza faini hiyo.
Faini hiyo ambayo inahitaji kulipwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ni zaidi ya faida ya mwaka mmoja ya MTN nchini Nigeria.
Nigeria imekuwa ikilazimisha makampuni ya mawasiliano kuwasajili wateja wao kutokana na hofu kuwa, kadi ambazo hazijasajiliwa zinaweza kutumiwa na makundi ya kigaidi na wahalifu.

No comments:

Post a Comment