Misri yaufunga mtandao wa Facebook.
Maafisa nchini Misri wameufunga mtandao wa mawasiliano ya kijamii wa Facebook, ambao unawaunganisha zaidi ya watu milioni tatu. Wizara ya mawasiliano ya simu imesema kufungwa kwa mtandao huo hakuhusiani na sababu za kiusalama. Lakini baadhi ya wakosoaji wamesema mtandao huo umefungwa wiki chache tu kabla ya kutimia miaka mitano tangu lilipozuka vuguvugu la mapinduzi ya umma katika mataifa ya Kiarabu, ambalo lilisababisha kuondolewa madarakani Rais Hosni Mubarak. Majukwaa ya mawasiliano ya mitandao ya kijamii yalionekana kama chombo muhimu wakati wa vuguvugu la mwaka 2011 na ilifungwa mara moja, wakati maandamano ya umma kuipinga serikali ya Mubarak yakipamba moto. Majukwaa hayo yalitumika kuandaa maandamano na kueneza ukosoaji dhidi ya serikali.
No comments:
Post a Comment