WATU 10 WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA NDEGE INDIA.
Watu 10 wameripotiwa kufa baada ya ndege ndogo ya jeshi kuanguka leo muda mfupi baada ya kupaa mjini New Delhi, India. Watu hao wakiwemo wafanyakazi wa ndege walikuwa katika ndege ya Super King, ambayo ni ya kikosi cha usalama wa mipakani. Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Delhi kwenda kwenye mji wa mashariki wa Ranchi. Mara baada ya kuruka, ilianguka karibu na uwanja wa ndege. Hakuna taarifa zozote rasmi zilizothibitishwa kuhusu wahanga. Aidha, chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
No comments:
Post a Comment