Saturday, December 26, 2015

Tetemeko la ardhi lakumba Afghanistan


PeshawarImage copyrightEPA
Image captionWatu 17 wamejeruhiwa mjini Peshawar, Pakistan
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.3 limekumba maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan, na kuathiri maeneo ya mbali hadi India.
Kwa mujibu wa Idara ya Utafiti wa Jiolojia ya Marekani kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa mkoa wa Badakhshan, karibu na mpaka wa Pakistan na Tajik.
Haijabainika iwapo kulikuwa na majeruhi eneo hilo, lakini watu 17 walijeruhiwa katika mji wa Peshawar, nchini Pakistan.
Mamia ya watu waliuawa eneo lilo hilo 26 Oktoba baada ya tetemeko jingine la ardhi kutokea.
Eneo hilo limekuwa likikumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi inayosababishwa na mgongano wa maeneo bara ya India na Eurasia.
Maeneo hayo yanaingiliana kwa kiwango cha sentimeta 4-5 kila mwaka.
Mwaka 2005, tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.6 kwenye vipimo vya Richter katika eneo la Kashmir, linalotawaliwa na Pakistan, liliua watu zaidi ya 75,000
Na Aprili mwaka huu, Nepal ilikumbwa na tetemeko mbaya zaidi nchini humo lililoua watu 9,000 na kuharibu nyumba 900,000.

No comments:

Post a Comment