Thursday, December 17, 2015

Marekani yapandisha kiwango cha riba


Benki Kuu ya Marekani imepandisha kiwango kikuu cha riba kwa alama ya robo ya asilimia kwa mara ya kwanza tangu 2006.
Kwa muda wote tangu mtikisiko wa uchumi nchini humo mwaka 2008 riba ilibaki kuwa kati ya 0% na 0.25%. Lakini sasa kiwango kikuu cha riba kitakuwa kati ya 0.25% na 0.5%.
Imekuwa ni kipindi kisicho cha kawaida katika sera za uchumi nchini Marekani na sasa hatua ya benki kuu imeweka alama ya kuanza kurejea kwa kiwango cha riba cha kawaida.
Imechukua takriban miaka saba kwa Benki hiyo kuchukua uamuzi huo wa kuongeza kiwango hicho kidogo cha riba. Hii ni sehemu ya kujikinga na hatari ya mfumuko wa bei kwa siku zinazokuja.
Hata hivyo hatua hiyo sasa inatia mashaka kwa uchumi wa nchi zinakuwa kwa haraka kama Uturuki, Brazili na Afrika Kusini.
Kuna uwezekano kuwa uamuzi huo sasa utawafanya baadhi ya wawekezaji kuondoa fedha zao ili kufaidika na riba hiyo kubwa nchini Marekani.
Pia hatua hiyo itadhoofisha sarafu ya nchi hizo na kuongeza gharama za mikopo.
Aidha pia hatua inatarajiwa kuyumbisha mfumo wa fedha japo nchi tajiri zinaweza kuimarika zaidi kama zitahimilli msukuko huo tafauti na hapo awali.

No comments:

Post a Comment