Uli Hoeness atumai kuachiwa huru mwez Machi.
Mahakama ya Augsburg katika jimbo la Bavaria, inatafakari uwezekano wa kumuachia huru Mmiliki wa kilabu ya Bayern Munich Uli Hoeness ambaye anatumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu gerezani kwa kosa la ukwepaji kodi. Hoeness ambaye ametumikia nusu ya kifungo hicho huenda akaachiwa huru tarehe 29 mwezi Februari mwakani kwa kupewa msamaha. Mahakama hiyo ya Augsburg hapo jana imethibitisha imepokea ombi la kumzingatia mmiliki huyo wa Bayern Munich kuachiwa huru. Hoeness mwenye umri wa miaka 63 alihukimiwa mnamo mwezi Machi mwaka jana baada ya kukiri kukwepa kodi ya takriban euro milioni 28.5. Gazeti la Bild limeripoti kuwa amelipa kodi hiyo aliyokwepa pmaoja na riba na kwasababu ilikuwa mara ya kwanza kwake kukutikana na hatia, huenda mahakama ikamsamehe.

No comments:
Post a Comment