Tuesday, December 8, 2015

 SENTENSI SABA ZA KILICHOJADILIWA NA CCM KUHUSU MOTO WA SERIKALI   YA RAIS MAGUFULI.
Jana December 07 2015 kamati kuu ya Chama cha CCM ilifanya kikao kikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Leo Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amefanya mkutano leo kuzungumzia yale ambayo yamezungumzwa ndani ya kikao hicho cha jana.
Pongezi kwa Serikali ya Rais Magufuli >>>> “Kama Chama tunaunga mkono juhudi zao na tunaahidi kuwaunga mkono.. Kamati kuu inaunga mkono juhudi za Rais wa sasa kuhusu mamlaka za mapato kusimamiwa ipasavyo, juhudi hizi za awamu ya tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana, kamati inawataka wahusika wote watoe ushirikiano kwa wahusika wote“- Katibu Mkuu CCMAbdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akimpigia salute Rais Magufuli.
Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akimpigia salute Rais Magufuli.
Kamati kuu kama ilivyoagizwa na ilani ya uchaguzi, tumefurahi kuona wanasimamia matumizi yasiyo ya lazima kwa Serikali, lazima tumuunge mkono.. pia tunawataka wanaCCM na wananchi wote kumuunga mkono Rais kwa kufanya kazi kwa maarifa na uadilifu, kujituma ili kujenga nchi yetu“- Abdulrahman Kinana.
Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia.
Rais MagufuliWaziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia.
Hayo ni machache kutoka kwenye Kikao cha CCM walivyojadili Serikali ya Rais Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa Kassimkwenye kasi yao.

No comments:

Post a Comment