Monday, December 14, 2015

Waziri wa zamani Rwanda kukaa jela miaka 47


PaulineImage copyrightGetty
Image captionPauline Nyiramasuhuko amehukumiwa pamoja na mwanawe Shalom
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imeamua waziri mmoja wa zamani wa Rwanda atumikie kifungo cha miaka 47 jela kwa mchango wake mauaji ya kimbari ya 1994.
Pauline Nyiramasuhuko ni mmoja wa washtakiwa sita waliokuwa wamekata rufaa kwenye mahakama hiyo maalum ambayo imemaliza kazi yake.
Alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani awali, lakini mahakama ikaamua kupunguza adhabu dhidi yake, sawa na adhabu dhidi ya Arsène Shaim Ntahobali na Elie Ndayambaje.
Kesi hizo zilikuwa za mwisho kusikizwa na mahakama hiyo kabla ya kufungwa rasmi baada ya kusikiza kesi dhidi ya washukiwa wa mauaji hayo kutoka mjini Arusha, Tanzania kwa miaka 21.

No comments:

Post a Comment