Friday, December 11, 2015

Mwanajeshi ashambuliwa na duma akipiga picha

Kasi

 
Duma wanaweza kukimbia kwa kasi ya kilomita 104 kwa saa
Jeshi la wanahewa la Afrika Kusini limesema duma wawili, ambao hufugwa kwenye kambi ya jeshi hilo ili kufukuza wanyama wengine njia ya kutumiwa na ndege kupaa, wamemshambulia afisa wa jeshi.
Msemaji wa jeshi hilo Marthie Visser amesema kupitia taarifa kwamba duma hao waliingia eneo ambalo ndege huegeshwa katika eneo la Makhado.
Mwanajeshi aliyekuwa kwenye zamu aliwaona na kujaribu kuwapiga picha na hapo ndipo wakamshambulia.
Mwanajeshi huyo hakujeruhiwa vibaya na ameachiliwa kutoka hospitalini.
Wanyama hao hawatafukuzwa katika kambi hiyo.
Bi Visser alisema kambi hiyo, iliyo kaskazini mwa Afrika Kusini, imezingirwa na mbuga za wanyama na duma hao husaidia kudhibiti ongezeko la wanyama mwitu.

No comments:

Post a Comment