Sunday, December 20, 2015


Sanders aomba msamaha kumdukua Hillary Clinton


Image copyrightAFP
Image captionSanders aomba msamaha kumdukua Hillary Clinton
Mgombea anayewania tikiti ya chama cha Democratic nchini Marekani Bernie Sanders amekiri na kuomba msamaha kwa aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni na pia mgombea mwenza
Bi Hillary Clinton kwa kudukua taarifa za upigaji kura, zilizo tayarishwa na kikosi cha kumfanyia kampeini Bi Clinton.
''Kwa hakika hii sio njia ninayopenda wala kampeini ya aina hii hainifurahishi kamwe,''alisema Sanders.
Kundi la kumfanyia kampeini Sanders, limelaumiwa kwa kudukua taarifa za upigaji kura, zilizo tayarishwa na kikosi cha kumfanyia kampeini Bi Clinton.
Bwana Sanders amemuomba msamaha Bi Clinton kwa kikosi chake kudukua taarifa za siri za upigaji kura iliyokusanywa na kikosi cha Bi Clinton.
Katika mahojiano ya moja kwa moja ya runinga, wagombea hao walitofautiana kuhusiana na sera za mataifa ya kigeni, ugaidi na swala la kudhibiti silaha zinazomilikiwa na raia nchini Marekani.
Huku pia maswala ya uchumi yaliibua mjadala mkubwa, kiwangi cha juu cha matibabu na elimu.
Image copyrightAP
Image captionMjadala wao wa mwisho wa moja kwa moja wa runinga, ulifanyika katika jimbo la New Hampshire.
Mjadala wao wa mwisho wa moja kwa moja wa runinga, ulifanyika katika jimbo la New Hampshire.
Aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Bi Hilary Clinton, anasalia kuwa kidedea katika kinyang'anyiro hicho.
Wafuasi wake wanakilaumu chama cha Democratic kwa kumpendelea Bi Clinton.
Kundi la Bwana Sanders, limelaumiwa kwa kudukua taarifa za upigaji kura, zilizo tayarishwa na kikosi cha kumfanyia kampeini Bi Clinton.
Mwaandishi wa BBC huko New Hampshire, anasema kwamba Bi Clinton anaweza kuamua kuzungumzia swala hilo au kuendelea kuzungumzia swala tata la ugaidi duniani.

No comments:

Post a Comment