Monday, December 14, 2015

Ashtakiwa kwa kukosoa chama tawala China


Image copyrightAFP
Image captionPu Zhiqiang
Mwanasheria wa haki za binadamu nchini China ameshtakiwa nchini humo kwa kukikosoa chama tawala.
Mwanasheria huyo maarufu Pu Zhiqiang mashtaka dhidi yake yanahusishwa na taarifa alizotuma katika mitandao ya kijamii kukikosoa chama hicho cha kikomunist.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema hakukuwa na nafasi ya kuachiliwa huru kwa Bwana Pu na inaelekea atafungwa kifungo cha miaka hadi nane gerezani.
Makundi ya haki za binadamu kimataifa wameelezea kesi hiyo kama ni ya kisiasa.

No comments:

Post a Comment