Sunday, December 13, 2015

Mwanamke wa kwanza achaguliwa Saudi Arabia


Raia wa Saudi Arabia wameweka historia kwa kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa mwakilishi wao katika uchaguzi uliofanyika hapo jana.
Tume ya uchaguzi ya Saudia Arabia imetangaza.
Salma bint Hizab al-Oteibi alichaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza mwakilishi wa wilaya katika jimbo la Mecca.
Japo matokeo ya uchaguzi huu yanaendelea kutangazwa tangazo hilo limeibua hisia miongoni mwa wenyeji.
Hii ndio iliyokuwa mara ya kwanza wanawake kupiga kura na kushiriki kama washindani.
Maafisa wa Serikali walisema kuwa wanawake 130,000 walijiandikisha kupiga kura, ambayo ni sehemu moja kwa kumi ya wapiga kura wanaume.

Kuna zaidi ya wagombeaji 1,000 wanaong'ang'ania viti mbalimbali katika uchaguzi huo.
Wanawake hawa walikuwa wakifanya kampeni zao huku wamesimama nyuma ya pazia au wakati mwingine wanawakilishwa na mwanamume.
Wanawake kadhaa wa Saudi Arabia wamepongeza uchaguzi huo kama hatua muhimu.
Hata hivyo wengine wanasema kuwa hauna umuhimu wowote kwa sababu maisha yao yana vizuizi vingi kama vile kutoruhusiwa kuendesha magari.

No comments:

Post a Comment