Tuesday, December 22, 2015


Wanajeshi sita wa Marekani wameuawa katika shambulizi lililotokea karibu na kambi ya Bagram nchini Afghanistan. Jumuiya ya Kujihami ya NATO, imethibitisha jana kwamba wanajeshi hao walikuwa wakishika doria wakati mshambuliaji aliyejitoa mhanga alipowagonga na pikipiki yake iliyokuwa na mabomu. Hilo ni shambulizi baya kabisa dhidi ya vikosi vya kimataifa tangu mwezi Agosti. Wanajeshi wawili wa Marekani na mmoja wa Afghanistan walijeruhiwa. Aidha, shirika la habari la Reuters liliripoti jana kuwa wilaya moja mjini kabul ilishambuliwa kwa makombora matatu huku kombora moja likianguka karibu na eneo la kuingilia kwenye Ubalozi wa Marekani, katika uwanja wa Masoud. Shambulizi hilo limetokea siku chache baada ya ubalozi wa Uhispania kuzingirwa katika shambulizi lililosababisha mauaji ya Wahispania wawili na kiasi ya polisi wanne wa Afghanistan.

No comments:

Post a Comment