Saturday, December 5, 2015

Obama: Hatutayumbishwa na shambulio

 

Obama amesema Marekani iko imara
Rais Barack Obama amesema Marekani haitayumbishwa na shambulio la Jumatano katika mji wa San Bernardino, California.
"Sisi tuna nguvu. Tuko imara," amesema kwneye hotuba yake ya kila wiki kupitia redio, akisema inawezekana kwamba watu wawili waliofyatua risasi na kuua watu 14 katika mji huo walikuwa wameingizwa kwenye itikadi kali.
Syed Rizwan Farook, 28, na mkewe Tashfeen Malik, 27, walitekeleza mauaji hayo kabla ya kuuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika yao na polisi.
FBI wanachunguza kisa hicho kama kitendo cha ugaidi.
Kundi la wapiganaji wanaojiita Islamic State Jumamosi lilisifu shambulio hilo na kusema lilitekelezwa na “watu wawili wanaounga mkono Islamic State".
Taarifa hiyo iliyopeperushwa kupitia redio ya IS ya al-Bayan haikutoa ishara zozote kuhusu kuhusika kwa kundi hilo kwenye shambulio hilo katika sherehe ya Krismasi kituo cha Inland Regional Center.
"Tunajua kuwa Isil (IS) na makundi mengine ya kigaidi yanawahimiza watu – kote duniani na hata nchini mwetu – kutenda vitendo vibaya vya mauaji, wakati mwingine kivyao,” Bw Obama amesema.
"Sote, serikali, idara za usalama, jamii, viongozi wa kidini, tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja kuzuia tusipotoshwe na itikadi hizi za chuki.”
Tashfeen Malik na Syed Farook 
Malik 
Familia za Farook na Malik zimeeleza kushtushwa na vitendo vya wawili hao na kusema hawakudhani wawili hao wangeweza kutekeleza mauaji.

No comments:

Post a Comment