Sunday, December 13, 2015

Aung San Suu Kyi, aiga mfano wa Magufuli



Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, leo alivaa glavu na kuokota taka katika tarafa yake.
Majuzi bi Suu Kyi, aliwaomba wabunge wa chama chake waliochaguliwa hivi karibuni, kwamba waokote takataka, kama sehemu ya kampeni ya kufanya usafi nchini.
Chama chake cha NLD kilishinda viti vingi katika uchaguzi uliofanywa mwezi uliopita.
Serikali ya sasa ya kijeshi, imeteua kamati kusimamia shughuli ya kukabidhi madaraka chama cha bi Suu Kyi.
Uchafu ni tatizo la taifa nchini Myanmar, ambayo haina mfumo hasa wa kukusanya taka na kuzitupa.

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi mpya kuchukua majukumu ya kuweka usafi.
Rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli, aligonga vichwa vya habari kote duniani alipochukua jukumu la kusafisha mji mkuu wa Dar es Salaam Tanzania badala ya kuongoza sherehe za kuadhimisha sikuu ya kitaifa.

No comments:

Post a Comment