Wednesday, December 23, 2015


Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema ghasia katika miji ya Wakurdi nchini Uturuki zimeongezeka huku wanajeshi wakitumia nguvu, ikiwemo matumizi ya vifaru kuwakabili wanamgambo wa kikurdi. Makundi ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wa kikurdi nchini Uturuki wamesema raia kadhaa wameuawa katika mashambulizi hayo na kusababisha maelfu ya wengine kuyahama makaazi yao. Serikali ya Uturuki imetangaza amri ya kutotoka nje katika baadhi ya miji ya Wakurdi kusini mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha raia wa maeneo hayo kukosa, vyakula, maji na umeme. 

No comments:

Post a Comment