Tuesday, December 8, 2015

Watu milioni 10 wanahitaji chakula Ethiopia


Image caption
Serikali ya Ethiopia imeonya kuwa watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa kufuatia ukame mkubwa uliokumba maeneo mengi nchini humo.
Ukame huo unakisiwa utaathiri takriban watoto milioni 6 ambao watahitaji msaada wa chakula kuanzia mwezi ujao.
Serikali tayari imeanza kugawanya chakula cha msaada kwa ushirikiano na mpango wa chakula duniani WFP kufuatia ukame ulioathiri mazao msimu uliopita.
Aidha serikali hiyo ya Ethiopia imetenga dola milioni 200 kwa shughuli hiyo ya kutoa chakula kwa waathiriwa.
Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children linasema kuwa ukame huu ndio mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Ethiopia kwa kipindi cha miaka 50.
Image copyrightAFP
Image captionSave the Children inakisia kuwa itahitaji dola bilioni nne kukidhi matakwa ya zaidi ya watu milioni 10 .
Hata hivyo kutokana na idadi kubwa ya wahasiriwa serikali na wadau wamelazimika kuomba msaada wa kitaifa.
Save the Children inakisia kuwa itahitaji dola bilioni nne kukidhi matakwa ya zaidi ya watu milioni 10 .
Zao lingine linatarajiwa mwezi juni mwakani hata hivyo matumaini ya wengi huenda yakaambulia patupu kufuatia mabadiliko ya tabia nchi na tishio la ukame unaotokana na El Nino.

No comments:

Post a Comment