Wednesday, December 30, 2015

Uchaguzi wa urais waanza Afrika ya Kati


Uchaguzi

Image copyrightAFP
Image caption
Uchaguzi huu umeahirishwa mara nne mwaka huu

Raia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanapiga kura leo katika uchaguzi wa urais na ubunge ambao unalenga kurejesha uthabiti nchini humo.
Wagombea 30 wanawania urais katika uchaguzi huo ulioahirishwa mara kadha.
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa wanatumai kuzuia marudio ya ghasia zilizokumba kura ya maamuzi kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huu wiki tatu zilizopita.
CAR imeathiriwa pakubwa na mapigano tangu wapiganaji wa Kiislamu wa Seleka wachukue mamlaka Machi 2013.
Wapiganaji wa Kikristo waliojulikana kama anti-Balaka baadaye walivhukus silaha na kuanza kupigana na wa Seleka.
Januari 2014, serikali ya mpindo iliundwa ikiongozwa na kaimu rais Catherine Samba-Panza.
Uchaguzi mkuu nchini humo umeahirishwa mara kadha tangu Februari 2015 kutokana na machafuko na kuchelewa kwa maandalizi ya uchaguzi.
Wagombea watatu ndio wanaoaminika kuwa na ushawishi mkubwa.
Wawili kati yao, Martin Ziguele na Anicet Dologuele, waliwahi kuhudumu kama mawaziri wakuu chini ya rais wa zamani marehemu Ange-Felix Patasse.
Wa tatu, Karim Meckassoua, ni Mwislamu aliyehudumu kama waziri chini ya Rais Francois Bozize hadi walipoondolewa mamlakani na wapiganaji wa Seleka mwaka 2013.

CARImage copyrightAFP
Image caption
CAR ni moja ya nchi alizozuru Papa Francis kwenye ziara yake ya kwanza Afrika Novemba

Wachunguzi wanasema huenda kukafanyika duru ya pili ya uchaguzi, sana mwishoni mwa Januari.
Uchaguzi pia unafanyika kuchagua wabunge 105.
Baada ya kuchukua uongozi, waasi wa Seleka walimuweka uongozini Michel Djotodia, akiwa kiongozi wa kwanza Mwislamu katika taifa hilo lenye Wakristo wengi.
Lakini baada ya shinikizo kutoka kwa viongozi wa kanda na mkoloni wa zamani Ufaransa, Bw Djotodia aling’atuka na nafasi yake ikachukuliwa na Bi Samba-Panza.
Bw Djotodia na Bw Bozize wote wamo uhamishoni na wamewekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa na Marekani kwa kuchangia machafuko nchini humo.

No comments:

Post a Comment