Wednesday, December 23, 2015


Wanaume wawili wamekamatwa kuhusiana na jaribio la shambulizi la kigaidi karibu na eneo la Orleans kusini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Polisi imesema washukiwa hao walipanga kufanya mashambulizi yanayolenga asasi za kiusalama. Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema mashambulizi hayo yaliyotibuliwa na shirika la ujasusi la Ufaransa, yalikusudia kuwalenga maafisa wa usalama katika eneo la Orleans. Wanaume wawili raia wa Ufaransa wenye umri wa miaka 20 na 24 mtawalio walikamatwa tarehe 19 mwezi huu. Mmoja wa washukiwa hao aliwaambia wachunguzi kuwa walipanga kuwashambulia wanajeshi, polisi na wawakilishi wa serikali. Cazeneuve amewaambia wanahabari kuwa washukiwa hao wawili walikuwa na mawasiliano na mwanamgambo ambaye ni raia wa Ufaransa aliyeko Syria na polisi wanchunguza iwapo walipokea maagizo ya kufanya mashambulizi kutoka kwa jihadi huyo.

No comments:

Post a Comment