Amnesty yalaumu mashambulizi Syria
Kikundi cha kampeni kinachoongozwa na shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International kimesema kwamba kinao ushahidi kwamba mashambulio ya anga yanayofanywa na Urusi nchini Syria tangu mnamo mwezi September yameua maelfu ya raia, na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.
Katika taarifa iliyokuwa katika mtindo wa mahojiano yalikuwa na mashuhuda,madaktari na vikundi vya kutetea haki za binaadamu, Amnesty ilithibitisha mashambulizi sita.Na katika kila shambulio kulikuwa na raia kadhaa ambao ni majeruhi ingawa ni dhahiri hakukuwa na uharibifu katika kambi za jeshi zilizo kuwa karibu na makaazi ya watu.
Katika taarifa hiyo pia kuna maelezo ya hospitali na makaazi ya watu kugongwa ama kuharibiwa vibaya ikiwemo masoko na misikiti kadhaa.Ingawa taarifa kutoka mjini Moscow,Urusi zimeikana taarifa hiyo na kudai kwamba lengo lao kuu ni kundi la wanamgambo wa Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Amnesty hawakuishia hapo walidokeza pia uwepo wa matumizi haramu ya mabomu na uharibifu wa majengo na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya mashambulizi hayo ya anga.
No comments:
Post a Comment