Ardhi yapasuka na kumeza magari 12
Wataalamu wa
jiolojia wameitwa kuchunguzwa ni jinsi gani ardhi ilipasuka na kumeza
magari 12 katika maegesho ya magari jijini Mississippi.
Shimo
kubwa, la urefu wa futi 400 (120m) na upana wa futi 35 (11m), lilitokea
baadaye Jumamosi katika eneo la Meridian, karibu na barabara kuu ya
Alabama.
Eneo hilo limekuwa likipokea mvua kubwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kwa mujbiu wa gazeti la Meridian Star.
Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho, na wahandisi wanatarajiwa kudadisi uthabiti wa ardhi eneo hilo leo.
Bw
Buck Roberts, tmkurugenzi wa usalama wa umma eneo la Meridian, aliambia
gazeti hilo kwamba hilo halionekani kuwa shimo la kawaida ambalo
hutokana na sehemu inayohifadhi maji chini ya ardhi kukauka na ardhi
kuporomoka.
No comments:
Post a Comment